#2 YOTE NI MAPYA
SIKU YA 1. Alikwenda zake akifurahi – Matendo 8:26-39
Mwafrika huyu tajiri mwenye mamlaka alikabiliana na tukio la kuvutia mno! Baada ya kusafiri kwa miezi hadi Yerusalemu akimtafuta Mungu wa kweli, akinunua gombo lililoandikwa kwa mkono lenye ujumbe uliotolewa na nabii Isaya, akiwa njiani kurudi nyumbani Mungu anakutana naye. Filipo mtumishi mwaminifu wa Mungu akikimbia kwenye joto la mchana kando ya gari la kukokotwa la huyo mwafrika, anamsikia akisoma kwa sauti kifungu kikuu kinachohusu mwana-kondoo mtumishi anayeteseka. Analipokea kwa furaha ombi kupanda kwenye gari na kumweleza huyo mtunza hazina wa Kiethiopia maana ya ya kifungu hiki cha Maandiko. Mara huyu msafiri wa Kiafrika anamwamini Yesu Masihi, anaomba abatizwe na kwa mara nyingine ana “kwenda zake akifurahi.”
Lifikirie hilo:
Ilimgharimu kiasi gani huyu Mwafrika mwenye mamlaka kuitafuta habari njema ya uzima wa milele ndani ya Yesu? Ilikugharimu kiasi gani wewe?
Mungu alimwangalia mtafutaji huyu na akamtumia Filipo katika
wakati unaofaa amwonyeshe njia mpya. Mungu alikuongozaje ulipokuwa ukiitafuta kweli? Na wewe uliipata ile furaha kuu ukiwa katikati ya mazingira magumu yaliyokukabili?
MAOMBI:
Bwana Mungu, Ninakushukuru kwa kuniongoza pote na kunionyesha njia ya furaha katika kumfuata Yesu. Ninakushuru kwa watu uliowaleta kwenye maisha yangu wakanielezea kweli
yako, walionitia moyo kuweka tumaini langu ndani yako, na walioniombea ili nionyeshwe njia iliyo sahihi. Sasa kwa kuwa niko kwenye Njia ya Yesu ninakuomba uwe kiongozi wangu wa kila siku, na unisaidie kukufuata kwa furaha. Amina.