#5 MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU
VITU SABA AMBAVYO NI CHUKIZO KWAKE BWANA
Soma Mithali 6:16-19 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Leo tupo katika somo la tano kuhusu vitu ambavyo Mungu anavichukia. Tutaangalia maana ya "miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu.
MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU
Tukiamini na kufahamu Neno la Mungu, tunajua anatuambia tena na tena kubaki mbali na uovu. Kukataa uovu na kutokubali uovu. Lakini hata hivyo, kuna watu ambao wako tayari kujiunga na watendao uovu. Katika Mithali 1:10-15 tunaambiwa kuhusu kundi la "wenye dhambi" ambao wanasubiri kwa uvamizi kuwaua watu na kuwaibia mali zao. Mungu anaichukia miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu. Mithali 1:15-16 inasema "Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao, maana miguu yao huenda mbio maovuni. Miaka michache iliyopita kulikuwa ajali mjini ya Morogoro, Tanzania. Lori kubwa ya petrol ilipinduka na petrol ilikuwa inamwagika barabarani. Watu wengi walishika ndoa na kontaina mbali mbali ili waibe petroli lile. Mtu mmoja akapanda juu ya injini ya lori ili aibe betri. Alipokuwa anaondoa betri, cheche ikatokea na moto ililipuka na watu 100 wakafa pale pale na 47 wengine walichomwa vibaya na moto na kupata majeuri mabaya. Kwa nini? Watu wakaona nafasi kuiba kwa hiyo walijiunga na wengine na walipoteza maisha yao. Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu ni chukizo wa Bwana.
Katika Isaya 59 Mungu anatuambia tabia za wale ambao hawafuati maagizo ya Mungu. Mstari wa saba inasema "Miguu yao hukimbilia mabaya." Na sisi Wakristo tunaweza "kukimbilia" uovu pia tusipolinda na kupima mazoea yetu. "Kukimbilia maovu" yanaweza kutokea kwa njia mbali mbali. Je, unasubiri kwa hamu wiki baada ya wiki kuangalia programu ya TV isiyofaa? Inachekesha na kuwafurahia watu lakini labdha mavazi yao au mazumgumzo yao hayafai kwa Wakristo. Unakimbilia video mpya yasiofaa? Sisi sote tunapaswa kulinda macho yetu. Tukiweka mambo yasiyofaa mbele ya macho yetu na macho ya familia zetu, tunaweza kuwasha tamaa za mwili na kufungua mlango ya kukimbilia maovu. Watu wangapi siku hizi wanajiunga na michezo ya kamari ile waweze kupata bahati? Wakishinda mara moja katikati ya mashindano mia, wanatangaza ushindi wao kana kwamba ni kitu cha kawaida. Wengine wanakimbilia michezo hizi na kupoteza hela na matumizi wa nyumbani. II Yohana 1:8-" Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda."
Hata kanisani siku hizi tunaona watu ambao wanahubiri "mafanikio ya maisha" ukihudhuria kanisa lao au mpango wao. Watu wanakimbilia sana kwa mahubiri haya. Lakini Mungu anatuita kuwa watakatifu, watenda kazi ya Mungu na kutopenda fedha. I Watimotheo 6:10 inasema " Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha."
Sisi sote tunahitaji kupima njia zetu. Kila siku tujihoji nakuhakikisha njia za mapito yetu. Zaburi 25:4 inasema " Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako." Mithali 3:6 inasema " Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."
Badala ya kukimbilia maovu, tuikimbilie haki. Mithali 13:14 inasema " Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Zaburi 25:4 inasema " Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako." Ikiwa tuko tayari kumfuata Mungu, yeye yuko tayari kutuonyesha. Tuwe tayari kuacha njia za maovu na kujifunze njia zake.
Ombi:
Bwana Yesu, nashukuru kwa Neno lako niliopewa ili nijue njia zako. Unisaidie kusimama dhidi ya maovu, nisivutwe na wengine kukimbilia maovu kwa namna lo lote. Naomba unihoji. Unionyeshe njia ninazopaswa kufuata. Katika jina la Yesu Kristo. Amina