Podcast episode 12: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #2 IMEANDIKWA NA MARY SMITH

Sep 9, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith


hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyomyepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Wakati uliopita tulianza kujifunza kuhusu vitu ambavyo ni chukizo kwake Mungu. Katika o r o d h a ya M i t h a l i 6 : 1 6 - 1 9 , t u l i j i f u n z a k u h u s u k i t u c h a k w a n z a , m a c h o y a k i b u r i . L e o tunaangalia kitu cha pili, ulimi wa uwongo.


# 2 ULIMI WA UONGO

Neno la Mungu linataja "uwongo" mara 166. Ikiwa inatajwa mara nyingi kama hivyo, bila shaka ni muhimu. Tena, kumbuka

chukizo kwa Bwana; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake." Zaburi 34:13 "Uuzuie ulimi wako na mabaya na midomo yako na kusema hila." Ndoa ngapi zimeharibika kwa sababu mmoja au mwingine anasema uwongo? Marafiki wangapi wameachana kwa sababu ya uwongo? Sijui mara ngapi nipo pamoja na wengine na mtu moja anajibu simu na kusema. "ndiyo, nipo njiani" na kumbe, anasimama pale pale na kuongea! Uwongo!

•Pia katika biashara nimeshuhudia uwongo mwingi. Wanasema itakuwa tayari siku fulani wakati ambapo wanajua haiwezekani. Mungu anachukia uwongo.

Katika kitabu cha I Wafalme 21:1-16 tunasoma kuhusu Nabothi. Mfalme Ahabu alitaka kununua shamba lake na alikataa. Yezebeli aliwalipa watu kusema uwongo ili aweze kuchukua shamba lile. Nabothi aliuawa kwa sababu ya ushahidi wa uwongo. Yesu Kristo aliuawa kwa sababu ya ushahidi wa uwongo wa Mafarisayo. Baada ya kufufuka kwake Yesu, maaskari walilipwa kusema mwili wa Yesu uliibwa na wafuasi wake. Uwongo unaangamiza vitu vingi na huharibu maisha ya wengi.

Kinyume cha uwongo ni ukweli. Ukweli ni Yesu. Yohana 14:6 "Yesu alisema "Mimi ndimi

njia, na kweli na uzima." Wakolosai 3:9-10 inasema "Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawa sawa na mfano wa Muumba wake." Tulipookoka, tumevaa maisha mapya. Tunapaswa kuacha m a m b o ya dunia hii na kuvaa m a m b o mapya. Wakolosai 4:6 unatuambia "Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu." Tuwe kama mwandishi wa Zaburi 141 mstari wa 3. Yeye alimwomba Mungu maneno haya - "Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu." Tupo vitani. Neno la Mungu linatuambia kuwa tayari kupinga hila za shetani. Waefeso 6:14 inatuambia "mmejifunga kweli kiunoni." Maneno yetu yaaminike. Maneno yetu yategemewe. Mathayo 5:37 inasema "Maneno yenu yawe ndiyo, ndiyo; siyo siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu."

Maombi yetu yawe kama Zaburi 39:1- "Nalisema, nitazitunza njia zangu. Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu."


Kuomba:

Mungu Baba, naomba unisaidie kutosema uwongo. Weka askari kinywani kwangu. Niwe mtu wa kweli. Nisamehe kwa kusema uwongo. Naomba unisaidie kukupendeza kwa usemi

wangu. Katika jina la Yesu, Ukweli wetu, Amina.

More From Podcast

Podcast Episode 20: Interview with Phelistas part 2
Nov 11, 2024    elizabeth
Podcast episode 19: Interview with Phelistas part 1
Oct 28, 2024    Audio by Elizabeth Calmes
Podcast episode 18: Interview with Liz
Oct 20, 2024    Audio by Elizabeth Calmes
Podcast episode 17: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #7 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Oct 13, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith
Podcast episode 16: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #6 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Oct 6, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith
Podcast episode 15: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #5 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Sep 29, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith
Podcast episode 14: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #4 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Sep 22, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith
Podcast episode 13: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA #3 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Sep 15, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, written by Mary Smith
Podcast Episode 11: VITU SABA AMBAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA: #1 IMEANDIKWA NA MARY SMITH
Sep 2, 2024    Audio by Tina Omolo, Audio by Elizabeth Calmes, Written
Podcast Episode 10: Phelistas part 1
Aug 25, 2024    Audio by Elizabeth Calmes
Podcast Episode 9: Interview with Lindsey about Anxiety
Aug 21, 2024    Audio by Elizabeth Calmes
Podcast Episode 8: Tabitha part 5
Aug 12, 2024    Audio by Elizabeth Calmes