#4 Upendo definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Kwanza

ni Upendo


Upendo ni tunda lililotangazwa kwanza katika orodha hii. Pengine ni kuonyesha umuhimu kwa Mkristo kuonyesha sifa hii katika maisha yake kila wakati. Mtu ambaye anaenenda na Roho Mtakatifu atakuwa anaishi maisha yake katika upendo. Atampenda Mungu sana na atapenda binadamu. Upendo huu hujali watu wengine juu ya mwenyewe. Watu wengine huweza kuvutiwa nayo. Upendo huu haumaanishi upendo au penzi ya mwili. Upendo huu unao asili yake katika Mungu na unapatikana tu katika Wakristo wanaoishi na kuenenda kwa Roho Mtakatifu.