#12 Amani Definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Roho

ni Amani:


Amani ya kiroho ina maana iliyo nzito zaidi ya utulivu wa akili na roho ya mtu. Katika Biblia amani kutoka Mungu ni amani ambayo haiwezi kuelezwa na binadamu kwa kuwa inadumu. Vilevile ni amani inayotafuta jinsi ya kuwaletea wengine utulivu. Mkristo mwenye amani halisi atawasaidia wenzake ili wawe na amani katika mahusiano yao na jamii zao. Yaani, hujitahidi kuleta na kuendeleza amani kila anapoenda. Amani ya kibinadamu inabadilika siku kwa siku kutokana na hali tofauti za maisha. Amani kutoka kwa Mungu ni hali ambayo ni imara na kuendelea katika roho ya mtu kwa kuwa imewekwa humo na Mungu. Mtu wa amani ataweza kuvumilia dhoruba za maisha kwa kuwa anao uhakika kwamba Mungu atamsaidia kuzipitia.