#6 Upendo Lesson 2
Somo la Pili: Upendo wa Mkristo
Kumbukumbu la Torati (KKT) 7:9, Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu;
Rum 8:28, Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Kol 3:12-14, 12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, 13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
1Pet 4:8, Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
1Yoh 3:18, Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
1Yoh 4:7, Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
1Yoh 4:8, Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
1Yoh 4:12, Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
1 Yoh 4:18, Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
1Yoh 4:19, Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.
1Yoh 4:20, Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.