#10 Furaha lesson 2

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Furaha: Somo la Pili 


Zab 118:24, Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia. 


Zab 119:111, Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu." 


Zab 126:2-3, 5-6, 2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. 3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi… 5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. 6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake. 


Mith 17:22, Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa. 


Yer 15:16, Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.


Hab 3:17-18, 17 Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; 18 Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. 


Luk 1:47, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; 


Luk 15:10, Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye. 


Yoh 15:10-11, 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 


Yoh 16:22, Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.