#9 Furaha Lesson 1

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Furaha: Somo la Kwanza 


1 Nya 16:26-27, 26 Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. 27 "Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. 


Zab 4:7, Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. 


Zab 5:11, Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima . Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia." 


Zab 16:11, Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.


Zab 19:8, Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. 


Zab 30:5, Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. 


Zab 33:21, Maana mioyo yetu itamfurahia, Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu. 


Zab 51:8,12, Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. 


Zab 70:4, Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. 


Zab 97:11, Nuru imemzukia mwenye haki, Na furaha wanyofu wa moyo.