#8 Furaha Definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Pili: ni Furaha


Furaha kama tunda la Roho haimaanishi hali yako ya kufurahi kutokana na jambo zuri lililotokea maishani mwako. Pengine umepata kazi, au kuponywa na ugonjwa, au kupata hela ghafula na umefurahi na kuchangamka. Maana hii si maana ya furaha kwenye Biblia. Bali maana ya furaha katika Biblia ina maana nzito zaidi. Furaha halisi inategemea kumjua Mungu, yaani mtu mwenye furaha anamfurahia Mungu kwa kuwa ameelewa hakuna kilicho bora zaidi kuliko Mungu. Watu Wakristo humshukuru Mungu kwa yote aliyowatendea. Furaha inatoka katika hali hii ya shukrani, pamoja na kumpenda na kupendwa na Mungu. Furaha ya namna hii hufurahi katika nyakati nzuri na nyakati mbaya. Ipo katika hali ya kuwa na uwingi na katika hali ya kuona hasara. Furaha hii haitegemee hali ya mtu, inadumu kwenye moyo wa mtu. Furaha hii inaeleweka na Wakristo tu kwa kuwa ni tunda la Roho Mtakatifu. Soma mistari inayofuata kujifunza zaidi juu ya tunda la furaha.