#24 Fadhili lesson 2

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Fadhili ya Mungu: Somo la Pili


Zab 6:4, Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.


Zab 13:5, Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.


Zab 23:6, Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.


Zab 25:7, Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.


Zab 26:11, Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili.


Zab 31:7, Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,


Zab 31:19, Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!


Zab 32:10, Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye Bwana fadhili zitamzunguka.


Hos 6:6, Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.


1Pet 2:1-3, 1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; 3 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.


1Pet 2:9, Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;