#25 Uaminifu definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Roho: ni Uaminifu


Mkristo mwaminifu huaminika, yaani hutegemeka. Maana yake ni, watu huweza kukuamini na neno lako; watu huweza kukusadiki katika kutimiza ahadi zako; watu huweza kukutegemea katika kutenda kama ulivyosema. Mkristo mwaminifu hatasema siri za marafiki, bali atakaa nayo kwa kimya. Mkristo mwaminifu atamwiga Mungu ambaye ni mwaminifu kabisa katika kila jambo. Tukisoma mistari ya uaminifu wa Mungu tutapata kuelewa jinsi ambavyo ni sharti tumwige yeye. Katika uaminifu wako, mwangalie mfano wako, yaani, Yesu, ili uelewe maana ya uaminifu halisi. Acha tabia hii kuwa ndani yako kwa uwingi ili watu huweza kukuamini wewe.