#27 Uaminifu wa Mungu lesson 2
Uaminifu wa Mungu: Somo la Pili
Zab 33:4, Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Zab 89:1, Fadhili za Bwana nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Zab 91:4, Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
Omb 3:23, Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
Rum 3:3-4, 3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa
Mungu? 4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
1 Kor 1:9, Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
Tit 2:9-10, 9 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, 10 wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote.
1Thes 5:23-24, 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.
Ebr 10:23, Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;
Ebr 11:11, Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
2 Thes 3:3, Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.
1 Yoh 1:9, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Ufu 19:11, Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.