#31 Kiasi definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Roho: ni Kiasi (Kadiri, Wastani)


Kiasi ni hali ya kuweza kujizuia katika hali yako yo yote. Katika fikra na matendo yako utaonyesha hali ya kiasi au kadiri au wastani. Mkristo mwenye kiasi hataishi maisha ya anasa ya ajabu atajizuia katika kupata kila anachokitaka. Kama mwandishi wa Mithali alivyomwomba Mungu akisema, Usinipe hali ya umaskini wala utajiri. Vilevile Mkristo mwenye kiasi ataridhika hali ya kawaida. Katika kushikwa na jazba na hisia fulani, huyu anajua jinsi ya kuzisimamia jazba zake ili zisimtawale. Wewe huweza kujua kwamba ukiwepo naye huyu mwenye kiasi utaona hakasiriki wakati wote. Hata katika hisia ya mapenzi huyu hujua jinsi ya kujizuia ili asifanye dhambi kwa kukubali hisia zisizofaa.