#28 Upole definition

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Tunda la Roho: ni Upole


Tunda la upole unamaanisha mtu ambaye ni mnyenyekevu. Upole haumaanishi mtu ambaye ni mdhaifu, bali ni mtu ambaye anaweza kuwa na tabia ya unyenyekevu katika matukio yote. Mkristo mpole akiongoza atafanya kwa unyenyekevu na upole. Mkristo huyu akipata hasira ataweza kujizuia asionyeshe hasira yake, aendelee katika hali ya utaratibu ingawa anasikia hasira. Mkristo mpole hulitii Neno la Mungu na kuliacha kuongoza tabia zake. Ni tabia iliyo kinyume (opositi) cha kiburi na hasira. Hata Yesu amejitambulisha kuwa mpole na myenyekevu wa moyo. Yeye aliacha mbinguni, alionyesha unyenyekevu kwa jinsi alivyokuja duniani kutembea na wenye dhambi na kuwafia msalabani. Hakuna unyenyekevu wala upole kama huo. Tumeitwa kumfuata na kufanana naye.