#26 Uaminifu wa Mkristo Lesson 1

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Uaminifu wa Mkristo: Somo la Kwanza


Zab 37:3, Umtumaini Bwana ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.


Zab 119:30, Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu.


Zab 145:18, Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.


Mith 11:13, Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.


Mith 12:22, Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.


Mith 14:5, Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.


Mith 20:6, Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?


Mith 25:13, Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.


Mith 25:19, Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.


Mith 28:20, Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.


1 Kor 4:1-2, Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. 2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.


1 Tim 1:12-13, 12 Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake; 13 ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.