#29 Upole somo 1

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Upole: Somo la Kwanza


Zab 22:26, Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao Bwana watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele.


Zab 25:9, Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.


Zab 37:11, Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.


Zab 147:6, Bwana huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.


Zab 149:4, Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.


Mith 15:1, Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.


Math 5:5, Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.


Math 10:16, Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.


Math 11:28-30, 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.


Gal 6:1, Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.


Fil 4:5, Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.