#32 Kiasi somo 1

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Kiasi: Somo moja


Mith 15:16, Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana, ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.


Mith 16:32, Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.


Mith 25:27-28, 27 Haifai kula asali nyingi mno; vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu. 28 Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.


Mith 29:11, Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.


Mith 30:7-9, 7 Mambo haya mawili nimekuomba; usininyime [matatu] kabla sijafa. 8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. 9 Nisije nikashiba nikakukana, nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, na kulitaja bure jina la Mungu wangu.


Rum 12:3,16, 3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani…16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.


1 Kor 9:25, Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.


1 Thes 4:3-5, 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.


1 Tim 2:9, Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.


2 Tim 1:7, Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.


Tit 2:11-12, Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;


Ebr 13:5-8, 5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. 6 Hata twathubutu kusema, bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? 7 Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni Imani yao. 8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo n ahata milele.