#23 Fadhili lesson 1

Written by Elizabeth Calmes, Audio by Elizabeth Calmes

Fadhili ya Mkristo: Somo la Kwanza


Zab 18:25, Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;


Zab 52:8, Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.


Zab 85:10-11, 10 Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana. 11 Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni.


Zab 89:2, Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.


Mith11:27, Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia.


Mith 21:21, Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima.


Dan 9:13, Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba Bwana, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake.


Hos 4:1, Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.


Hos 10:12, Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.


Hos 12:6, Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.


Luk 6:32-34, 32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. 33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.